Agutu alitiwa mbaroni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta baada ya kuwasili kutoka Somalia.
Polisi wanadai kuwa wawili hawa wamekuwa na mawasiliano na washirika wakuu wa Al Shabaab akiwemo Mohammed Kuno maarufu Dulyadin ama Gamadhere anayesakwa na polisi kwa madai ya kuhusika na mauaji ya Garissa.
Serikali imeahidi kima cha shilingi milioni 20 kwa yeyote atakayetoa habari kuhusu Dulyadin.
Balozi wa Tanzania nchini Oman Mh. Ali Ahmed Saleh (aliyebeba mtoto) akiwa na baadhi ya kundi la Watanzania 18 waliookolewa kutoka Yemen ambako hakukaliki kutokana na vita. Hapa wananchi hao wapo katika uwanja wa ndege wa Muscat wakiwa njiani kurejeshwa nyumbani.
Viongozi wa dini ya kiislamu kutoka jamii ya Kisomali humu nchini wameikashifu serikali kwa kufunga hawala zao licha ya wao kuhusika pakubwa katika kupiga vita mienendo ya kundi la Al-shabaab.
Viongozi wa dini ya kiislamu kutoka jamii ya Kisomali humu nchini wameikashifu serikali kwa kufunga hawala zao licha ya wao kuhusika pakubwa katika kupiga vita mienendo ya kundi la Al-shabaab.
Shekh Mohammed Osman amepuzilia mbali madai kuwa viongozi wa dini ya kiisilamu hawawajibiki kuzuia makundi yenye itikadi kali na kusisitiza kuwa serikali haioni juhudi zao.
Aidha wamepinga hatua ya serikali ya kuhusisha misikiti na makundi yenye itikadi kali na kusema kuwa hatua hii inarudisha chini imani ya waislamu katika kupinga harakati za makundi ya kigaidi.
Wakizungumza baada ya kikao cha mashauriano jijini Nairobi, viongozi hao wameahidi kuanza kampeni ya kuhamasisha vijana dhidi ya makundi yenye itikadi kali kama njia ya kuepuka kujiunga na kundi la Al-shabaab.
MAAFISA wa polisi mjini Nyahururu nchini Kenya usiku wa kuamkia Alhamisi walitibua mpango wa watu wasiojulikana wakionya jamii ya waislamu kuhama mjini humo.
Kulingana na mkuu wa polisi Nyandarua kaskazini Benjamin Onsongo, karatasi Zenye ujumbe wa kuwataka Waislamu waondoke mjini humo zilianza kusambazwa Jumapili iliyopita.
Onsongo alisema ilani hiyo iliipa jamii hiyo makataa ya siku saba kuhama mji huo kwani wamekataa kutambulisha maadui wanaoivamia nchi ya Kenya.
“Tumeanzisha uchunguzi na tumewaongeza maafisa wa polisi wanaoshika doria katika eneo hilo na nina uhakika kuwa tutawatia mbaroni wahusika,” alisema Bw Onsongo.
Viongozi wa kiislamu wakiongozwa na Imam wa msikiti wa Jamia mjini Nyahururu Sheikh Mohamed Huka pamoja na mwenyekiti wa muungano wa Waislamu kaunti ya Laikipia Sheikh Isaack Osman waliambia jamii ya waislamu mjini humu kutoogopeshwa na ilani hizo kwani maafisa wa polisi wanalishughlikia suala hilo.
Sheikh Mohamed Huka wa msikiti wa Jamia, Nyahururu akiwa na moja
ya vijikaratasi vilivyosambazwa mji wa Nyahururu Alhamisi vikiwataka watu wa
dini ya Kiislamu wahame mji huo
“Karatasi hizi zinasambazwa na watu wachache ambao wanataka kututawanya kwa misingi ya kidini lakini hatutakubali kugawanywa, ninaamini kuwa Nyahururu ni mji wa amani,” alisema Osman.
Sheikh Huka alisema kuwa jamii ya Waislamu imekubali kukumbatia mfumo wa Nyumba Kumi ili kuinua usalama na kuwauliza kuwa na subira huku maafisa wa polisi wakiendeleza uchunguzi

Mwili wa mwanamume huyo ulipatikana asubuhi ukinig’inia kwenye nguzo za transfoma hio huku nguo zake zikionekana kuwa zimeraruka.
OCPD wa Buruburu Richard Kerich alisema: “Mwanamume huyo alikanyaga nyaya zilizokuwa na umeme kupelekea kwake kuangukia nyaya zengine zenye umeme na kusababisha kifo chake.”
Mafuta ya transfoma yanaaminika kutumiwa katika kukaanga viazi ili kutengeza chipsi.
Polisi bado hawajabaini mtu huyo ni nani na mwili wake kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha jiji la Nairobi.
chanzo: jaridaleo































Rais Kikwete amewasili mjini Kahama kiasi cha saa nane mchana baada ya ndege yake kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi na kwa muda wa kiasi cha saa tatu ametembelea familia ambazo zimepata madhara makubwa zaidi kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa kiasi cha saa moja tu kuanzia saa nne usiku Machi 3, mwaka huu, 2015 na kuambana na upepo mkali na mawe.
Watu 47 walipoteza maisha, 112 wakaumia, nyumba 657 zikabomolewa ama kuharibiwa na kaya 468 kuathirika katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata na tokea siku ya maafa, Serikali imetoa huduma za dharura za chakula, sehemu za kulala, huduma za afya na huduma nyingine muhimu kwa binadamu.
Baada ya kupatiwa maelezo ya kina na uongozi wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali N. Lufunga, Rais Kikwete ameanzia ziara yake katika Kijiji cha Maghuhumwa, nyumbani kwa Bwana Masemba Maburi, ambaye alipoteza watoto watano katika maafa hayo. Rais Kikwete ametoa pole kwa wafiwa na kuzungumza na wananchi waliokuwepo kwenye msiba.
Bwana Maburi ambaye sasa anaishi katika nyumba ya jirani pamoja na familia yake na familia nyingine tatu amemweleza Rais Kikwete jinsi nyumba mbili ambako watoto hao na mama yao walipokuwa wamelala zilivyoanguka na mama huyo akalazimika kukimbilia nje kwa nia ya kutafuta msaada lakini watoto wakazidiwa na kupoteza maisha.
“Sijawahi kuona mvua kubwa, kali na yenye upepo mkali kiasi kile katika maisha yangu. Mvua ilianza saa nne usiku na ikanyesha kwa muda mfupi sana, nyumba zikaanguka ama kubomolewa. Jameni tusaidie kwa sababu tumekwazika,”Bwana Maburi amemwambia Rais Kikwete.
Baada ya kutoka katika Kijiji cha Maghuhumwa, Rais Kikwete amekwenda katika Kijiji cha Nhumbi ambako amempa pole Bwana Zacharia Limbe na familia yake ambayo ilipoteza wajukuu wanne katika maafa hayo ya mwanzoni mwa mwezi huu.
Akiwa nyumbani kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembea na kujionea makazi mapya ya dharura ya familia ambayo yamejengwa kwa msaada wa Serikali.
Baada ya kuondoka kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembelea eneo la makazi ya walimu wa Shule ya Msingi ya Mwakata, ambako walimu hao wamehifadhiwa katika fremu za maduka kutokana na athari za maafa hayo. Rais Kikwete amewapa pole walimu hao na kuwaambia: “Pole sana. Tuko pamoja. Tutaendelea kusaidiana kuona jinsi gani mnavyoweza kurejea katika maeneo yenu ya makazi ya kawaida.”
Rais Kikwete ataondoka kesho, Ijumaa, Machi 13, 2015, kurejea Dar es Salaam baada ya ziara hiyo maalum ya siku mbili katika Mkoa wa Shinyanga.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Machi, 2015





…………………………………………………………………………………….

Kauli hiyo ameitoa wakati akikabadhi soko la Tumbe Wilaya ya Micheweni kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazni Pemba , ambalo limejengwa na kampuni ya Ngogo ya Iringa na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 712.
Aidha waziri jihad amewataka wananchi wa Wilaya ya Micheweni kulitumia soko hilo kwa kufuata mila , silka na tamaduni wa watu wa Tumbe .















