Viongozi wa dini ya kiislamu kutoka jamii ya Kisomali humu nchini
wameikashifu serikali kwa kufunga hawala zao licha ya wao kuhusika
pakubwa katika kupiga vita mienendo ya kundi la Al-shabaab.
Viongozi wa dini ya kiislamu kutoka jamii ya Kisomali humu
nchini wameikashifu serikali kwa kufunga hawala zao licha ya wao
kuhusika pakubwa katika kupiga vita mienendo ya kundi la Al-shabaab.
Shekh Mohammed Osman amepuzilia mbali madai kuwa viongozi wa dini ya
kiisilamu hawawajibiki kuzuia makundi yenye itikadi kali na kusisitiza
kuwa serikali haioni juhudi zao.
Aidha wamepinga hatua ya serikali ya kuhusisha misikiti na makundi
yenye itikadi kali na kusema kuwa hatua hii inarudisha chini imani ya
waislamu katika kupinga harakati za makundi ya kigaidi.
Wakizungumza baada ya kikao cha mashauriano jijini Nairobi, viongozi
hao wameahidi kuanza kampeni ya kuhamasisha vijana dhidi ya makundi
yenye itikadi kali kama njia ya kuepuka kujiunga na kundi la Al-shabaab.
0 comments:
Post a Comment