Hatimaye kundi la kwanza lililo na wakenya 15 waliyokuwa nchini Yemen
wanatarajiwa kuwasili katika uwanja wa jomo kenyetta hii leo.
Kulingana na mkuregenzi wa masuala ya mataifa ya kigeni humu nchini
Washington Oloo ni kuwa serikali imekuwa ikiwasiliana na mataifa ya
china na India ilikusaidia kuwahamisha wakenya kutoka maeneo yaliyo
athirika zaidi na ghasia.
Oloo ameongeza kwa kusema kuwa zaidi ya wakenya 5000 wamekwama katika
taifa la yemen huku 53 wakitorokea nchi jirani ya Saudi Arabia.
Aidha takriban wakenya 250 wanaishi katika vitongoji vya mji mkuu wa
Sanaa nchini humu ikilinganishwa kuwa ni moja la eneo lilikumbwa na vita
hivyo.
Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwezi huu maeneo mengi nchini Yemen yameweza kuathirika na ghasia.
0 comments:
Post a Comment