Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal na Waziri wa Miundombinu Dk. John Magufuli,Kamanda wa polisi Kanda maalum ya Daresalaam Suleiman Kova, Mkuu wa mkoa huo Said Mecky Sadick wamenusurika katika ajali ya Helkopta wakati akikagua uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua kubwa katika jiji hilo.
Viongozi hao akiwemo mpiga picha wa Shirika la Utangazaji la TBC, George Kasembe wamepatiwa matibabu kwa majeraha waliyoyapata na wameendelea na ziara yao ya kuangalia athari za mvua..
Kiasi ya watu 10 wakiwemo watoto wadogo wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la dar es salaam pamoja na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu ya madaraja na nyumba za makaazi.
Kamanda wa kanda maalum Dar es salaam Suleiman Kova mapema aliarifu kuwa hali sio nzuri jijini humo na kuwataka wananchi kuchukuwa tahadhari kwenye makazi yao na kupunguza mizunguko isiyo ya lazima kutokana na njia nyingi kuwa na mashimo.






0 comments:
Post a Comment