
Baadhi ya wanachama wa Chama cha
Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na wananchi wkishiriki matembezi ya
amani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno
jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) na wanachama wa
Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno iliyofanyika katika viwanja
vya Salender Bridge Club jana jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo
uliambatana na matembezi ya hiari yalioyoanzia katika viwanja hivyo na
kupitia Barabara ya Diomond Jubilee kabla ya kurudi uwanjani hapo
kupitia barabara ya AlhasanMwinyi na Kauli mbiu ya wiki ya Afya ya
Kinywa ni “Tabasamu la Maisha” Katikati ni Rais wa Chama Cha Madaktari
wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro na wa mwisho kulia
ni Rais Mteule wa Chama hicho Dkt. Ambege Mwakatobe.

Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akipeana mkono na
Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna
Carneiro (kulia) jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno.

Baadhi ya Wanachama wa Chama cha
Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) na baadhi ya wananchi
waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno
wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (hayupo pichani)
jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiangalia baadhi
ya machapisho yanayohusu Afya ya Kinywa na Meno kwenye banda lililowekwa
katika Viwanja vya Salender Bridge Club jana jijini Dar es Salaam
alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa
na Meno. Kushoto ni Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno
Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro.

Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (wapili kutoka
kushoto) akiwa katika matembezi ya amani ikiwa ni katika hfla ya
uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama wa Chama cha
Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na wananchi wkishiriki matembezi ya
amani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno
jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini/WHVUM.
0 comments:
Post a Comment