Serikali kuendelea kuandaa mazingira bora ya wavuvi Zanzibar


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe Abdilah Jihad Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kuandaa mazingira bora ya wavuvi ikiwa ni pamoja na kujenga  masoko  ya kisasa ili kuimarisha sekta ya uvuvi na kuzalisha ajira kwa wananchi . Amesema kuwa wananchi wengi wa Visiwa vya Zanzibar wanategemea sekta ya Uvuvi kuendesha shughuli zao za uchumi na kueleza kwamba jumla ya watu 34,000 wamejiajiri kupitia sekta ya uvuvi ambapo kupatikana kwa masoko ya kisasa kutaongeza ajira kwa wananchi .
Kauli hiyo ameitoa wakati akikabadhi soko la Tumbe Wilaya ya Micheweni kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazni  Pemba , ambalo limejengwa na kampuni ya Ngogo ya Iringa  na kugharimu zaidi ya  shilingi milioni 712.
Aidha waziri jihad amewataka wananchi wa Wilaya ya Micheweni kulitumia soko hilo kwa kufuata  mila , silka na tamaduni wa watu wa Tumbe .
“Tunatambua kwamba soko hili liko sehemu za mkusanyika wa watu wengi kutoka sehemu tofauti za Pemba , hivyo basi mnatakiwa kusimamia na kufuata mila , silka na tamaduni za wenyeji wa hapa ili kusiwepo na mporomoko wa maadili ya jamii ” alisisitiza Jihad . Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman amewashauri wavuvi wa Wilaya ya Micheweni kuhamasishana kulitumia soko hilo ili liweze kutumika na kukuza uchumi wao na Taifa kwa Ujumla .
Mkuu huyo wa Mkoa ameitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoa kipaombale cha kwanza kwa wakaazi wa Tumbe nakushauri kwamba uteuzi wa vijana kujiunga na chuo cha Uvuvi  zielekezwe kwa wakaazi wa Tumbe .
” Hizi nafasi za vijana kujiunga na chuo cha Uvuvi ambazo Wizara mmeanza kuzitoa naomba vijana wa Tumbe nao wapewe kipaombele cha pekee ili kuwafanya wakiridu waweze kuliboresha soko hili  ” alishauri Mkuu wa Mkoa .
Akitoa taarifa za ujenzi wa Soko hilo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw Kassim Gharib Juma amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2014  jumla ya Tani 30,000 wenye thamani ya bilioni 106 na wamevuliwa Unguja na Pemba .
Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuwafanya vijana kujiajiri wenyewe kupitia sekta ya Uvuvi na tuko mbioni kukamilisha mipango ya kuwaandaa wavuvi kuweza kufikia bahari kuu kwa ajili ya uvuvi .
Ameeleza kwamba hilo litafikiwa kutokana na azma za Rais Shein za kutoka kuiboresha sekta ya Uvuvi kwa kuwapatia vifaa na dhana za kisasa za uvuvi ambazo zitawafanya walitumie eneo la bahari kuu .
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment