Agutu alitiwa mbaroni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta baada ya kuwasili kutoka Somalia.
Polisi wanadai kuwa wawili hawa wamekuwa na mawasiliano na washirika wakuu wa Al Shabaab akiwemo Mohammed Kuno maarufu Dulyadin ama Gamadhere anayesakwa na polisi kwa madai ya kuhusika na mauaji ya Garissa.
Serikali imeahidi kima cha shilingi milioni 20 kwa yeyote atakayetoa habari kuhusu Dulyadin.
Balozi wa Tanzania nchini Oman Mh. Ali Ahmed Saleh (aliyebeba mtoto) akiwa na baadhi ya kundi la Watanzania 18 waliookolewa kutoka Yemen ambako hakukaliki kutokana na vita. Hapa wananchi hao wapo katika uwanja wa ndege wa Muscat wakiwa njiani kurejeshwa nyumbani.
Viongozi wa dini ya kiislamu kutoka jamii ya Kisomali humu nchini wameikashifu serikali kwa kufunga hawala zao licha ya wao kuhusika pakubwa katika kupiga vita mienendo ya kundi la Al-shabaab.
Viongozi wa dini ya kiislamu kutoka jamii ya Kisomali humu nchini wameikashifu serikali kwa kufunga hawala zao licha ya wao kuhusika pakubwa katika kupiga vita mienendo ya kundi la Al-shabaab.
Shekh Mohammed Osman amepuzilia mbali madai kuwa viongozi wa dini ya kiisilamu hawawajibiki kuzuia makundi yenye itikadi kali na kusisitiza kuwa serikali haioni juhudi zao.
Aidha wamepinga hatua ya serikali ya kuhusisha misikiti na makundi yenye itikadi kali na kusema kuwa hatua hii inarudisha chini imani ya waislamu katika kupinga harakati za makundi ya kigaidi.
Wakizungumza baada ya kikao cha mashauriano jijini Nairobi, viongozi hao wameahidi kuanza kampeni ya kuhamasisha vijana dhidi ya makundi yenye itikadi kali kama njia ya kuepuka kujiunga na kundi la Al-shabaab.
MAAFISA wa polisi mjini Nyahururu nchini Kenya usiku wa kuamkia Alhamisi walitibua mpango wa watu wasiojulikana wakionya jamii ya waislamu kuhama mjini humo.
Kulingana na mkuu wa polisi Nyandarua kaskazini Benjamin Onsongo, karatasi Zenye ujumbe wa kuwataka Waislamu waondoke mjini humo zilianza kusambazwa Jumapili iliyopita.
Onsongo alisema ilani hiyo iliipa jamii hiyo makataa ya siku saba kuhama mji huo kwani wamekataa kutambulisha maadui wanaoivamia nchi ya Kenya.
“Tumeanzisha uchunguzi na tumewaongeza maafisa wa polisi wanaoshika doria katika eneo hilo na nina uhakika kuwa tutawatia mbaroni wahusika,” alisema Bw Onsongo.
Viongozi wa kiislamu wakiongozwa na Imam wa msikiti wa Jamia mjini Nyahururu Sheikh Mohamed Huka pamoja na mwenyekiti wa muungano wa Waislamu kaunti ya Laikipia Sheikh Isaack Osman waliambia jamii ya waislamu mjini humu kutoogopeshwa na ilani hizo kwani maafisa wa polisi wanalishughlikia suala hilo.
Sheikh Mohamed Huka wa msikiti wa Jamia, Nyahururu akiwa na moja
ya vijikaratasi vilivyosambazwa mji wa Nyahururu Alhamisi vikiwataka watu wa
dini ya Kiislamu wahame mji huo
“Karatasi hizi zinasambazwa na watu wachache ambao wanataka kututawanya kwa misingi ya kidini lakini hatutakubali kugawanywa, ninaamini kuwa Nyahururu ni mji wa amani,” alisema Osman.
Sheikh Huka alisema kuwa jamii ya Waislamu imekubali kukumbatia mfumo wa Nyumba Kumi ili kuinua usalama na kuwauliza kuwa na subira huku maafisa wa polisi wakiendeleza uchunguzi