Wawili Wafikshwa Kotini Kwa Madai ya Kufadhili Al Shabaab

Mfanyibiashara maarufu Zadock Ainea Agutu na sheikh Ahmed Mursal ‘Sudan’ kutoka Mandera wamefikishwa mahakamani hii leo kwa madai ya kufadhili wanamgambo wa Al Shabaab.
Agutu alitiwa mbaroni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta baada ya kuwasili kutoka Somalia.

Polisi wanadai kuwa wawili hawa wamekuwa na mawasiliano na washirika wakuu wa Al Shabaab akiwemo Mohammed Kuno maarufu Dulyadin ama Gamadhere anayesakwa na polisi kwa madai ya kuhusika na mauaji ya Garissa.
Serikali imeahidi kima cha shilingi milioni 20 kwa yeyote atakayetoa habari kuhusu Dulyadin.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment