![]() |
Ismail Jussa aeleza chanzo, historia na athari zake kwa walioshiriki Asisitiza Katiba ya Zanzibar itashika hatamu. |
Dodoma.
Muundo wa Muungano ni kati ya sura za Rasimu ya Katiba ambazo zimezua
mjadala mzito kwa wajumbe wa Bunge la Katiba, hasa baada ya kuwapo kwa
mgawanyiko wa makundi yenye msimamo tofauti.
Kamati
ya Uongozi ya Bunge hilo ilipanga Sura ya kwanza na ya Pili kuwa sura
za awali ambazo zitajadiliwa na kamati 12 za bunge hilo, ikiwa ni hatua
ya kwanza kabla ya kuingizwa katika mjadala wa Bunge zima.
Mjadala
huo ni pamoja na kitendo cha Baraza la Wawakilishi kufanya marekebisho
ya katiba yake mwaka 2010 yaliyohusisha kumpa mamlaka zaidi rais wa
Serikali ya Mapinduzi na kutangaza visiwa hivyo kuwa nchi, uamuzi ambao
umetafsiriwa kuwa ni uvunjaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Hata hivyo, Ismail Jussa anaona kuwa wanaodai matatizo ya Muungano yameanza 2010, wanapotosha.
“Mwaka
wa mwanzo wa kuundwa kwa Muungano matatizo yalianza na mgogoro wa
mwanzo ulikuja wakati wa utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje,” anasema.
Anasema
wakati Zanzibar inaingia katika Muungano, Ujerumani Mashariki ilikuwa
ikiitambua na pia Tanganyika ilikuwa ikitambuliwa na Ujerumani
Magharibi.
Jussa,
ambaye pia ni mwakilishi wa Mji Mkongwe, anasema Ujerumani Magharibi
ilikuwa na sera yake kuwa nchi yoyote ambayo itaitambua Ujerumani
Mashariki, haitakuwa na mahusiano nayo ya kibalozi.
Anasema
baada ya Muungano, kulitokea mgogoro mkubwa baada ya Tanzania kuwa na
ofisi mbili za ubalozi. Mgogoro huo uliamuliwa kwa kufungwa kwa ofisi ya
ubalozi wa Ujerumani Mashariki.
“Palitokea
ugomvi mkubwa kwa kuwa Zanzibar ilikataa kufunga ubalozi wake nchini
Ujerumani Mashariki kwa sababu hao ni watu wao na wakati huo tayari
walikuwa wameshaanza kuimiminia misaada,” anasema.
Anasema mgogoro huo ulitishia kuvunjika kwa Muungano mwaka 1964, baada ya msimamo huo wa Zanzibar.
“Matokeo
yake baada ya mapambano makubwa kwa mara ya kwanza Ujerumani Magharibi,
ikawabidi kuvunja historia yao kwa kuruhusu Zanzibar kuendelea kuwa na
ofisi Ujerumani Mashariki,” anasema.
Jussa anasema pia mgogoro mkubwa wa sarafu ambao ulijitokeza mwaka 1965 uliohusu Benki Kuu.
0 comments:
Post a Comment