
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed
Shein (kulia) wakati alipojumuika na Mashekhe, Viongozi na Waislamu
mbali mbali katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume
Muhmmad S.A.W yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman
Mjini Unguja,(pichani) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi
akitia ubani kama ishara ya Ufunguzi wa Maulid hayo,[Picha na Ikulu.]

Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mama Zakia Bilali (katikati) akiwa na Wake wa makamo wa Pili wa rais wa
Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) na Mama Pili balozi Seif
(kulia) pamoja na Wake wa Viongozi mbali mbali na wananchi wa kawaida
wakijumuika katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume
Muhmmad S.A.W yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman
Mjini Unguja ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja
mfunguosita,[Picha na Ikulu.]

Akina Mama
kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na Vitongoji vyake wakiwa
katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja palipofanyika sherehe
za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W ambapo hufanyika
kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita na mgeni rasmi alikuwa Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed
Shein, [Picha na Ikulu.]


Ustadh salum Rashid kutoka Amani
Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Mlango wa Barzanji(4) wakati wa sherehe
za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.)
zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele
ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]
,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kabi (katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif
Sharif,Kadhi Mkuu wa zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) Waziri wa
katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary akifuataiwa na makamo wa Pili wa
Rais Alhaj Seif Ali Iddi wakisimaa kwa pamoja na waislamu wengine na
Viongozi wakati wa Kumswalia Bwana Mtume Muhammad S.A.W.katika sherehe
ya Maulid iliyofanyika jana viwanja vya Maisra Suleiman Mjini
Unguja,[Picha na Ikulu.]

Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali vya Quran
na Waislamu mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya
kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad S.A.W zilizofanyika jana katika Viwanja
vya Maisara Suleiman Mjini Unguja kama wanavyoonekanwa Pichani,[Picha na
Ikulu.]
0 comments:
Post a Comment