Hali ya taharuki imetanda eneo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa siku ya Jumapili baada ya milio ya risasi kusikika takriban saa tano na nusu mwendo wa asubuhi.
Mtu mmoja aripotiwa kufariki baada ya kupigwa risasi kutoka kwa nyuma.
Akithibitisha tukio hilo, mkuu wa Idara ya Upelelezi mjini Mombasa Henry Ondiek,alisema mwendazake alivamiwa alipokuwa akiingia mlango wa Kanisa la Maximum Revival lilioko eneo bunge la Mvita.
Haijabainika mpaka sasa sababu ya mauaji hayo huku polisi wakianzisha uchunguzi. Kufikia sasa, hakuna ishara yeyote kuonyesha shambulizi hilo lilikuwa ni la kikabila au kidini.
Bw. Ondiek alisema kulikuwa na maafisa wa polisi waliokuwa wamesimama lango la pili la kanisa hilo ambao walimfyetulia risasi mshambulizi huyo.
Jamaa huyo adaiwa kutoweka kwa miguu na kupotelea kwenye vichochoro vyembamba vya mtaa huo.
0 comments:
Post a Comment