MAELFU YA WATU WAKIWEMO VIONGOZI 40 WAANDAMANA NCHINI UFARANSA KUKASHIFU IMANI KALI


Charlie Hebdo 1
Waandamanaji wanaokisiwa kuwa milioni moja unusu wakiwemo viongozi 40 kutoka sehemu mbali mbali za dunia walitembea kwenye barabara za Jiji la Paris pamoja na waathiriwa 17 wa shambulizi la Charlie Hebdo ili kukashifu imani kali iliodhihirika siku tatu baada ya shambulizi hilo.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov.
Charlie Hebdo
Watu 12 wakiwemo wachoraji vibonzo wanne waliuwawa siku ya Jumatano huku mauaji yao yakigeuka na kuwa chombo cha kutetea uhuru wa kujieleza nchini Ufaransa na kwengineko ulimenguni.
Takriban polisi 2,000 na wanajeshi 1,350 walikuwepo kuwalinda waandamanaji hao walioimba “liberte” (“uhuru”) na “Charlie” wakihusisha mauaji yaliotendeka katika afisi za gazeti la Charlie Hebdo.
Walionekana kuinua bendera za Ufaransa huku wengine wakiimba wimbo wa taifa. Kikundi cha waandamanaji kilionekana kubeba muundo mubwa wa penseli ulioandikwa “not afraid” (“hatuogopi”) kwenye ubavu wake.
Maandamano mengine yalifanywa mjini Marseille ambao ni mji ulio na waisalamu wengi nchini Ufaransa. Meya wa mji huo Samia Ghali alisema kwamba maandamano hayo yalifanywa ili kudhihirisha haja ya kustahamiliana na kuishi pamoja kama jamii moja.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment