JARIDA LA RAUDHWAH

IMG_16827088238825


Hali ya taharuki imetanda eneo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa siku ya Jumapili baada ya milio ya risasi kusikika takriban saa tano na nusu mwendo wa asubuhi.
Mtu mmoja aripotiwa kufariki baada ya kupigwa risasi kutoka kwa nyuma.
Akithibitisha tukio hilo, mkuu wa Idara ya Upelelezi mjini Mombasa Henry Ondiek,alisema mwendazake alivamiwa alipokuwa akiingia mlango wa Kanisa la Maximum Revival lilioko eneo bunge la Mvita.
Haijabainika mpaka sasa sababu ya mauaji hayo huku polisi wakianzisha uchunguzi. Kufikia sasa, hakuna ishara yeyote kuonyesha shambulizi hilo lilikuwa ni la kikabila au kidini.
Bw. Ondiek alisema kulikuwa na maafisa wa polisi waliokuwa wamesimama lango la pili la kanisa hilo ambao walimfyetulia risasi mshambulizi huyo.
Jamaa huyo adaiwa kutoweka kwa miguu na kupotelea kwenye vichochoro vyembamba vya mtaa huo.


Charlie Hebdo 1
Waandamanaji wanaokisiwa kuwa milioni moja unusu wakiwemo viongozi 40 kutoka sehemu mbali mbali za dunia walitembea kwenye barabara za Jiji la Paris pamoja na waathiriwa 17 wa shambulizi la Charlie Hebdo ili kukashifu imani kali iliodhihirika siku tatu baada ya shambulizi hilo.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov.
Charlie Hebdo
Watu 12 wakiwemo wachoraji vibonzo wanne waliuwawa siku ya Jumatano huku mauaji yao yakigeuka na kuwa chombo cha kutetea uhuru wa kujieleza nchini Ufaransa na kwengineko ulimenguni.
Takriban polisi 2,000 na wanajeshi 1,350 walikuwepo kuwalinda waandamanaji hao walioimba “liberte” (“uhuru”) na “Charlie” wakihusisha mauaji yaliotendeka katika afisi za gazeti la Charlie Hebdo.
Walionekana kuinua bendera za Ufaransa huku wengine wakiimba wimbo wa taifa. Kikundi cha waandamanaji kilionekana kubeba muundo mubwa wa penseli ulioandikwa “not afraid” (“hatuogopi”) kwenye ubavu wake.
Maandamano mengine yalifanywa mjini Marseille ambao ni mji ulio na waisalamu wengi nchini Ufaransa. Meya wa mji huo Samia Ghali alisema kwamba maandamano hayo yalifanywa ili kudhihirisha haja ya kustahamiliana na kuishi pamoja kama jamii moja.




WILAYA YA MJINI.


WAUMINI WA DINI TAKIISLAM KOTE NCHINI WAMETAKIWA KUJITAHIDI KUTEKELEZA MAFUNDISHO YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KATIKA MAISHA YAO ILI KUPATA DARAJA YA UBORA HAPA DUNIANI NA KESHO SIKU YA MALIPO.

WITO HUO UMETOLEWA LEO NA UKHTI RAMLA RAMADHANI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WANAWAKE WAKIISLAM KATIKA UKUMBI WA SKULI YA SEKONDARI YA HAILESALASIE MJINI ZANZIBAR.

AKIZUNGUMZIA MADA KUHUSU KUPENDA MTUME MUHAMMAD S.A.W AMEBAINISHA KUWA HAKUNA MAANA YAKUMSWALIA PEKEE BALI NI KUTEKELEZA KWA VITENDO SUNA ZAKE NA KUEPUKA MAKATAZO YAKE.

HATA HIVYO UKHTI RAMLA AMEWATAKA WAISLAM KUDUMISHA NAKUYAENZI MATUKUFU YA DINI YAO YALIYOBAINISHWA KATIKA QUR-AN KWA KUYAFANYA KUWA NDIO DIRA YA MAISHA YAO.

MUHADHARA HUO WA WANAWAKE WAKIISLAM UMEHURIWA NA WAISLAM KUTOKA MJINI NA MAENEO JIRANI.



WOSHINTON.
MUHADHIRI MAARUFU WA KIISLAMU  NCHINI MAREKANI SAMAHATU SHEIKH ABU HAMZA AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA GEREZANI KATIKA MAHAKAMA MOJA MJINI NEW YORK KWA MADAI YAKUFANYA MAKOSA YA UGAIDI.
ALIM  HUYO ALIFUKUZWA NCHINI UINGEREZA MWAKA 2012 KUFUATIA KESI YA MUDA MREFU NA ALIPATIKANA NA HATIA MIEZI MINNE ILIYOPITA.
SHEIKH ABU HAMZA ALIPATIKANA NA HATIA KATIKA MASHTAKA KADHAA IKIWEMO NJAMA YA KUWATEKA NYARA WATU KUTOKA NCHI ZA MAGHARIBI IKIWEMO YEMEN MWAKA 1998 NA MAJARIBIO YA KUANZISHA KITUO CHA MAFUNZO YA UGAIDI KATIKA JIMBO LA OREGON NCHINI MAREKANI.
JAJI ALIYETOA HUKUMU YA KESI INAYOMKABILI MWANA WA CHUONI HUYO ALISEMA KUWA ABU HAMZA ALIKUWA AMEWACHOCHEA WATU WENGINE KUWAUA WALE WASIO WAISLAMU KAMA JUKUMU LA KIDINI NA KUSEMA KUWA ALIKUWA HATARI KWA JAMII.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum, Mhe Haji Omary Kheri, akiwana Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe Issa Haji Gavu, na Mkurugenzi Mkuu wa Shiriki la Bandari Zanzibar Ndg. Abdalla Juma, wakiwasili katika bandari ya Zanzibar kwa ajili ya Uzinduzi wa Tagi Mpya ya Shirika la Mabdari Zanzibar ilionunuliwa kupitia Mkopo wa Masharti Nafuu uliotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar wa Euro 4.43 milioni sawa na 9.7 Bilioni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum. Mhe Haji Omary Kheri, akikata utepe kuashiria kwa kulizindua rasmin Tagi ya kisasa ya Shirika la Bandari Zanzibar kwa kutowa huduma mbalimbali za Uokozi na kuvutia meli, uzinduzi huo umefanyika katika bandari ya forodhani., kushoto Naibu Waziri wa Miundombuni na Mawasiliano Zanzibar Mhe Issa Haji Gavu na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg Abdalla Juma. wakati akizundua Tagi hiyo. 
Tagi Mpya ya Shirika la Bandari Zanzibar ikiwa katika uzinduzi wake katika bahari ya forodhani baada ya kuzinduliwa. 
Tagi Mpya ya Shirika la Mandari Zanzibar inayoitwa SHUWARI, ikionesha moja ya huduma inayotolewa na Tagi hiyo wakati wa chombo kinapotokea na ajali ya moto ikirusha maji baharini wakati wa uzinduzi wake uliofanyika katika bahari ya forodhani, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
 Wageni waalikwa wakishuhudia Uzinduzi wa Tagi ya SHUWARI uliofanyika katika bandari ya abiria forodhani Zanzibar wakiangalia huduma za Tagi hiyo.

 Waalikwa wa Uzinduzi wa Tagi mpya wakifuatilia uzinduzi huo na kuangalia moja ya huduma inayotolewa na Tagi hiyo wakati wa uzinduzi wake.
 Mhe Waziri Omar Haji Kheri na Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe Dk. Sira Ubwa, wakishuka katika Tagi hiyo baada ya kuizundua na kuzunguka na kutowa huduma ya uokoaji kwa kumwaga maji kuonesha moja ya huduma za uzimaji moto ikitokea ajali ya moto kwa vyombo vya usafiri wa baharini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg Abdallah Juma, akisoma risala ya mafanikio wakati wa Uzinduzi wac Tagi ya Shuwari katika Bandari ya Forodhani Zanzibar, ikiwa ni mojaya Shamrashamra za kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

 Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Bandari Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Tagi Mpya ya Shirika hilo uliofanyika katika viwanja vya bandari ya forodhani Zanzibar. 
 Waheshimiwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg Abdallah Juma akitowa maelezo ya ununuzi wa Tagi hiyo mpya na kuishukuru Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ) kwa msaada wao wa Mkopo wa masharti nafuu kuweza kuinunua Tagi hiyo ili kuimarisha huduma katika Bandari ya Zanzibar kwa meli zinazitia naga katika Bandari ya Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar wakifuatila hafla ya Uzinduzi wa Tagi ya Shuwari iliozinduliwa katika Bandari ya Zanzibar ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar kilele chake kinafanyika 12 January 2015 katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
ulinzimkali

Na Tausi Ally
Kesi ya ugaidi inayowakabili viongozi 23 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu sasa kusikilizwa na Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda.
Awali kesi hiyo ambayo itatajwa Januari 13,2015 kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi, Hellen Liwa ambaye hata hivyo alijitoa.
Ni baada ya wakili wa washtakiwa hao wa ugaidi, Abubakar Salim kumtaka ajitoe kuisikiliza kesi hiyo ili iweze kupangiwa hakimu mwingine ambaye atatoa uamuzi juu ya hoja zao walizozitoa mahakamani hapo Septemba 19,2014.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ya ugaidi ni Sheikh Farid Hadi Ahmed ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mbuyuni Zanzibar, Fundi Ujenzi mkazi wa Koani Zanzibar, Noorid Swalehe na Jamal Nooridin Swalehe (38).
Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally na Juma Juma.
Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu kwa pamoja wanadaiwa kuwa walijihusisha na makosa hayo ya ugaidi kinyume na kifungu cha 27(c) cha sheria ya kuzuia ugaidi ya 2002.
Wanadai kuwa kati ya mwezi Januari 2013 na Juni 2014 walipanga njama ya kutenda makosa hayo ya kula njama za kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo vya kigaidi.
Katika kipindi hicho na maeneo tofauti nchini, Sheikh Farid na Sheikh Mselem Mselem wanadaiwa kuwaingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.
Sheikh Farid anadaiwa kuwa kwa makusudi na akijua alitoa msaada kwa watu hao wa kutenda vitendo vya kigaidi kinyume cha sheria na kuwahifadhi.
Chanzo: Mwananchi

Maandamano ya kuadhilishi Siku aliyozaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) wakipita katika barabara ya michezani kuelekea katika viwanja vya mnazi mmoja kusherehekea kwa kuzaliwac Mtume, Maandamano hayo ya Zafa yameazia katika Mskiti Mkuu wa Ijumaa Muembesauri Unguja na kumalizikiav katika viwanja vya mnazimmoja nas kupokelewa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Shekh. Omar Othman Makungu.
Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiwa katika maandamano ya Zafa kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad(S.A.W) Wakipita katika mitaa ya michezani na kuelekea katika viwanja vya mnazimmoja.
Wazazi wakiwa na Watoto wao katika maandamano ya kuadhimishi siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad.
Maandamano ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume yaliowashirikisha Wanavyuoni mbalimbali vilioko Unguja wakiwa katika maandamano hayo.kuelekea mnazimmoja kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika maandamano ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) 

Wanafunzi wa Madrasa wakisherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad kwa Dufu wakiwa katika maandamano wakielekea katika viwanja vya mnazimmoja Unguja. kuadhimisha siku hiyo tukufu.
Wanafunzi wa Madrasa mbalimbali wakishiriki katika maandamano ya Zafa ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtumu (S.A.W) katika viwanja vya mnazi mmoja Unguja.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Shekh, Omar Othman Makungu akipokea maandamano maalum ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammada(S.A.W), katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar.





Waumini wa Dini ya Kiislamu Zanzibar wakisherehekea Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) kwa maandamano yalioazia Masjid Mushawar Muembeshauri Zanzibar na kumalizikia katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu.


 
WAZIRI wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Mhe: Juma Duni Haji akiondoa kitambaa kuashiria kufungua kituo kipya cha kununulia karafuu, kilichopo Kilindi wilaya ya Chake Chake Pemba, kilichojengwa na ZSTC, ikiwa ni shamra shamra ya kutimia miaka 51 ya mapinduzi Zanzibar, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 BAADHI ya wananchi wa shehia ya Kilindi wilaya ya Chake Chake Pemba, wakimsilikiza Mkurugenzi mtendaji wa ZSTC Zanzibar, Mwahija Al-masi Ali akizungumza kwenye ufunguzi wa kituo kipya cha kununulia karafuu kwenye shehia hiyo, ikiwa ni shamra shamra ya kutimia miaka 51 ya mapinduzi Zanzibar, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 
KIKUNDI cha burudani cha Mkota ngoma cha Mkoani Pemba, kikitumbuiza kwa ngoma ya kibati, kwenye ufunguzi wa kituo kipya cha ununuzi wa karafuu shehia ya Kilindi wilaya ya Chake Chake Pemba, ikiwa ni shamra shamra ya kutimia miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzibar, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

WAZIRI wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Mhe: Juma Duni Haji, akizungumza  na wananchi wa shehia ya Kilindi wilaya ya Chake Chake Pemba, mara baada ya kukifungua kituo kipya cha kununulia karafuu, kilichopo shehiani humo, ambacho kilijengwa na ZSTC, ikiwa ni shamra shamra ya kutimia miaka 51 ya mapinduzi Zanzibar, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 


 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, alipofika eneo la Vikunguni kwa ajili ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika eneo hilo.
 Bango la mradi wa maji Vikunguni baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo.
 Baadhi ya wananchi pamoja na wakandarasi wa kampuni ya SINO-HYDRO LTD ya China, wakimsikiliza Maalim Seif wakati akiwahutubia wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika eneo la Vikunguni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na wananchi baada ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika eneo la Vikunguni. (Picha na Salmin Said, OMKR)
 
Na: Hassan Hamad (OMKR).
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuimarika kwa huduma za maji safi na salama nchini kutasaidia harakati za uzalishaji pamoja na shughuli za kiuchumi.
 
Umesema huduma hiyo pia husaidia kuokoa muda hasa kwa akinamama ambao mara nyingi hukabiliwa na jukumu la kutafuta maji kwa matumizi ya nyumbani.
 
Maalim Seif ametoa kauli hiyo wakati akifungua mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika eneo la Vikunguni jimbo la Wawi katika Wilaya ya Chake Chake, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Ameelezea kufarajika kwake kutokana na mradi huo kuanza kuwanufaisha wananchi wengi wa eneo hilo pamoja na vijiji jirani.
Amefahamisha  kupatikana kwa huduma hiyo ya uhakika, pia kutasaidia kujikinga na maradhi ya miripuko yakiwemo kipindupindu ambayo mara nyingi husababishwa na matumizi ya maji yasiyo salama.
 
Amewasisitiza wananchi kuulinda na kuutunza mradi huo, ili uweze kuwa endelevu na kuweza kutumika kwa muda mrefu.
 
Sambamba na hilo Maalim Seif amewataka wananchi hao kuepukana na uharibifu wa mazingira, ili kujikinga na athari za mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kusababisha kukauka na kuchafuka kwa vyanzo vya maji.
 
Ameeleza kuwa tayari vijiji kadhaa vya Zanzibar kikiwemo kijiji cha Nungwi, tayari kimekumbwa na athari hizo kwa visima vyao kuingiliwa na maji ya chumvi, na kuvitaka vijiji vyengine kuchukua tahadhari juu ya athari kama hizo.
 
Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdallah Shaaban, amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Zanzibar wanapata maji kwa asilimia 85 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
 
Amesema tayari ujenzi wa miradi ya maji mijini na vijijini umeshafikia asilimia 90 ambapo kazi ya usambazaji inaendelea vizuri.
 
Akisoma taarifa ya kitaalamu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Mustafa Aboud Jumbe, amesema zaidi ya shilingi bilioni mbili nukta tatu zimetumika kukamilisha mradi huo wa maji Vitongoji.
 
Amesema mradi huo ulioanzishwa mwaka 2011 ulijengwa chini ya ukandarasi wa kampuni ya SINO- HYDRO ya China, na uligharamiwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), UN-Habitat na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Amefahamisha kuwa Serikali imo katika utaratibu wa kulipatia ufumbuzi tatizo la umeme katika visima na matangi ya maji ili kuhakikisha kuwa huduma hiyo inapatikana kwa uhakika.
 
Katika risala yao wananchi hao wa Vikunguni wameishukuru Serikali na washirika wa maendeleo kwa kuwapelekea mradi huo ambao umeondosha kero ya upatikanaji wa maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.
 


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) wakati alipojumuika na Mashekhe, Viongozi na Waislamu mbali mbali katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,(pichani) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akitia ubani kama ishara ya Ufunguzi wa Maulid hayo,[Picha na Ikulu.]
 Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakia Bilali (katikati) akiwa na Wake wa makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) na Mama Pili balozi Seif (kulia) pamoja na Wake wa Viongozi mbali mbali na wananchi wa kawaida wakijumuika katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita,[Picha na Ikulu.]
 Akina Mama kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na Vitongoji vyake wakiwa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja palipofanyika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.]
Wanafunzi wa Madrasatul Dhuriyatul Islamia kutoka Kisiwani Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]


 Ustadh  salum Rashid kutoka Amani Wilaya ya Mjini Unguja akisoma  Mlango wa Barzanji(4) wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]
 ,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Kadhi Mkuu wa zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary akifuataiwa na makamo wa Pili wa Rais Alhaj Seif Ali Iddi wakisimaa kwa pamoja na waislamu wengine na Viongozi wakati wa Kumswalia Bwana Mtume Muhammad S.A.W.katika sherehe ya Maulid iliyofanyika jana viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali vya Quran na Waislamu mbali mbali waliohudhuria katika sherehe  za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad S.A.W zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja kama wanavyoonekanwa Pichani,[Picha na Ikulu.]
Next PostNewer Posts Previous PostOlder Posts Home