TATIZO LA UPUNGUFU WA WALIMU NA MADAKTARI LITAENDELEA

PEMBA.

MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA DADI FAKI DADI AMESEMA KUWA TATIZO LA UPUNGUFU WA WALIMU NA MADAKTARI LITAENDELEA KUZIKABILI NCHI ZINAZOENDELEA KUTOKANA NA ONGEZEKO LA WATU KATIKA NCHI HIZO LINALOSABABISHWA NA KUTOZINGATIWA SUALA LA UZAZI WA MPANGO .

DADI AMETOA KAULI HIYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZAZI , WANAFUNZI NA WALIMU WA SKULI ZA SEKONDARI ZA CHWAKA TUMBE , KINOWE NA TUMBE WAKATI WA ZIARA YAKE YA KUHAMASISHA MAENDELEO YA ELIMU KATIKA MKOA HUO .

AMESEMA KUWA IWAPO JAMII HAITAZINGATIA NA KUTOA KIPAOMBELE SUALA LA UZAZI WA MPANGO TATIZO HILO LA UPUNGUFU WA WALIMU NA MADAKTARI LITAENDELEA KUZIKABILI SEKTA YA ELIMU NA AFYA KATIKA NCHI HIZO IKIWEMO ZANZIBAR.

AMEWATAKA WAZAZI KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUKABILIANA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA WALIMU KATIKA SKULI ZAO PAMOJA NA KUWATUMIA VIJANA WALIOMALIZA VYUO VIKUU WALIOMO KATIKA MAENEO YAO .

AWALI MKUU HUYO WA MKOA ALIITAKA WIZARA YA ELIMU MKOA HUMO KUANDAA MIPANGO MADHUBUTI ITALAYO FANIKISHA KUPATIKANA KWA WALIMU WA MASOMO YA BIOLOGY NA PHYSICS KATIKA SKULI YA TUMBE NA CHWAKA .

KWA UPANDE WAKE AFISA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI MKOA WA KASKAZINI PEMBA NDUGU HASSAN SHEHA AMEWATAKA WAZAZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU KATIKA KUTAFUTA NJIA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO .
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment