Bismillahi-Rrahmani-Rrahim. Alhamdulillahi Rabbil Aalamiyn, waswalatu wassalam ‘alaa RasuliLlaahi. Amma ba’ad.
Assalamu ‘Alaykum wa RahmatuLlaahi wa Barakaatuh.
Anasema Allaah Subhaanahu wa Ta'ala:

}}وَأَقِمِ الصَّلاَةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّـيِّئَاتِ ذَلِكَ ذِكْرَى لِلذَّاكِرِينَ{{
{{Na shika Swalah katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanao kumbuka}} (11:114)
}}وَاسْتَعِينُواْ بِالصَّبْرِ وَالصَّلاَةِ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلاَّ عَلَى الْخَاشِعِينَ{{
{{Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu}} (2:45)
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ameturuzuku zawadi kubwa ambayo thamani yake haina mfano. Lakini kwa ajili ya uzoefu wetu juu yake, mara nyingi hatuipi cheo na heshima inayostahiki zawadi hiyo. Zawadi hiyo yenye thamani kubwa ni Swalah. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alituletea zawadi hii kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) alipopelekwa kwenye mbingu saba katika safari yake ya Mi’raaj. Kama tujuavyo, kwanza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   alipewa Swalah khamsini ambazo zilipunguzwa mpaka tano, zile tunazoziswali sasa; na kwa Ukarimu Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) tunapata fadhila ya zile Swalah khamsini vile vile, ilihali tunaswali tano. Subhana Allaah!
Kwa hivyo Swalah yetu, ambayo wengi wetu tunaichukulia kwa wepesi na kuipuuza, ina utukufu wa kukutana kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Inasemekana kuwa yale maneno tunayoyasema katika tashahhud ni kumbukumbu ya mawasiliano yaliyotokea baina ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Mola wake wakati huo wa Mi’raaj. Wa Allaahu A’alam. Kwa hivyo, kila tunapokaa kwenye tashahhud, inatupasa tuwe ni wenye kuzingatia utukufu wa kikao hicho.
Swalah ni mojawapo ya njia kubwa ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametutolea iwe ni hakikisho kuwa tunabaki kwenye njia ya Uislamu ambayo inaongoza kwenye Rehma Yake na Msamaha Wake, na kila zuri duniani na Aakhira. Kwa hakika, Swalah inatuunganisha na Mola wetu. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelinganisha Swalah na mto ambao mtu akioga ndani yake mara tano kwa siku, Hakika mtu huyo hatokuwa mchafu. Hivyo basi, Swalah zetu tano zinazuia kufungika kwa uhusiano baina yetu na Allaah. Kwa hivyo kuswali kwetu, daima kunafuta madhambi madogo yaliyotendeka baina ya kila Swalah. Allaah  (Subhaanahu wa Ta'ala)  Ametufaradhishia Swalah ili daraja zetu zipande, thawabu zetu zizidishwe, na madhambi yetu yadondoke kutoka kwetu, na kwa ajili yake Atutie Peponi na Atuokoe na Moto.
Walakini, Swalah ni kama upanga wenye makali pande zote mbili. Tukiihifadhi, itatupa mwangaza kwenye nyoyo zetu, makaburi yetu, na siku ya Kiama. Itatushuhudia wakati ambao tunahitaji shahidi ili tuokoke na adhabu ya Moto, kama tujuavyo kutoka kwa Yahya ibn Sa'id kwenye Muwatta: “kitendo cha kwanza kutizamwa siku ya Kiama ni Swalah, ikikubaliwa, basi vitendo vyengine vitaangaliwa, lau sio hivyo, basi vitendo vyote pia havitoangaliwa.” Lakini tukiipuza na kuitoa thamani, basi nayo itatoa ushahidi dhidi yetu, wakati ambao tunahitajia shahidi zaidi. Lazima tujihadhari tusiwe miongoni mwa watu wale ambao Allaah  (Subhaanahu wa Ta'ala) anawazungumzia katika Surat Maryam:
}}فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا{{
{{Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Sala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya}} (19:59)
Na tuzingatie maneno ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) : Jabir amesema, “nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akisema,
((Kitu ambacho kinasimama baina ya binaadamu na kutokuamini na shirki, ni kuacha Swalah))[Muslim]
Cheo cha Swalah katika dini ni kama mfano wa mlingoti wa nyumba, ukiwepo, nyumba itakuwa madhubuti na vifaa vyake vyote vitalingana mahali pake. Lakini isipokuweko, basi jengo lote litabomoka na kuwa halina maana.
Kulingana na hayo, ni muhimu kukumbuka kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hatuamrishi kuswali tu, bali Anatuamrisha tuimarishe Swalah, ambapo Mufassirun wote wamekubaliana kuwa kuimarisha Swalah, ina uzito zaidi kuliko kuswali tu rakaa tulizoambiwa. Kuimarisha Swalah ina maanisha shuruti zote za twahara, mahali pa kuswali, nguo, kibla, na mengineyo, yote ni lazima yatimizwe.
'Abdullaah bin Mas'uud amesema, "Yeyote anayetamani kukutana na Allaah  (Subhaanahu wa Ta'ala)  kesho, basi atunze Swalah hizi tano wakati muadhini unapoadhini Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  Alimuonesha Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  Sunnah zote za muongozo, na kuimarisha Swalah ni moja wapo. Ukiswali nyumbani kwako kama wanao kosa kuswali jama’a, umetupilia mbali Sunnah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) . Na ukitupa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) , huwezi kuongoka. Mumetuona sisi, na hakuna kati yetu ambao walikosa Swalah ya jama’ah isipokuwa wale wanafiki ambao unafiki wao ulikuwa unajulikana, au wale waliokuwa wagonjwa. Watu walikuwa wanakuja kuswali jama’ah huku wameshikiliwa na watu wawili mpaka wakasimamishwa kwenye safu”.
Swalah ni kitu ambacho hakiwezi kumalizwa kuzungumziwa, na vitabu vingi vimeandikwa juu yake, lakini ningependa kumalizia kwa kauli zifuatazo walizosema  baadhi ya Maulamaa waliotangulia,  kuhusu Swalah:
1)
"Kwa vile Allaah Anajua kuwa munachokeshwa na kitu mara moja,
Amezifanya namna kwa namna ibada zenu juu Yake.
Kwa vile Anajua kuwa muna pupa,
Amewakataza kuzifanya Ibada wakati mwengine.
Amefanya hivyo ili matamanio yenu yawe ni kuimarisha Swalah,
Sio kuswali tu!
Sio wote wenye kuswali wanaimarisha Swalah.
Swalah ni utakaso wa nyoyo,
Na mahali pa mazungumzo ya undani,
Baina ya mja na Mola wake.
 Viwanja vya siri vinaenea ndani yake,
Mianga  inaangaza na kumulika nuru zake.
Allaah Anajua nyinyi ni dhaifu,
Basi Amezifanya idadi za Swalah kidogo tu!
Anajua kuwa nyinyi ni wahitaji wa Rehma Zake nyingi.
Kwa hivyo amezidisha Neema Zake kwenu ndani yake"

2)
"Yeyote anayetamani kujiokoa nafsi yake, kujifurahisha moyo wake, kusitiriwa makosa yake, kupata Radhi za Mola wake, na moyo wake kupata uhai, lazima ampe heshima Anayostahiki Mola wake na asicheleweshe Swalah wakati unapoingia, na asijiruhusu kufanya hivyo. Wala asiswali peke yake wakati ambao anaweza kuswali jama’ah. Na bado tunaona watu wakichelewesha Swalah na kuswali peke yao ilihali wanaweza kuswali jama’a. Ni ubaya ulioje wanaoufanya hao. Tunawaona wamezama ndani ya mhangaiko, huzuni, taabu, na mateso. Hakika, chanzo cha yanayowapata ni kupuuza kwao kwa dini. Pia tunaona kuwa hawajui tofauti ya kuswali safu ya mbele wala ya nyuma. Sio kwa sababu hawajui, bali ni kwasababu ya kutojali dini. Hawajali kuhusu twahara pia.  Lakini ukweli ni kuwa, yeyote mwenye najisi, hana udhu, na ambae hana udhu, hana Swalah, na ambae hana Swalah, hana mazuri yoyote. Wa Allaahu A’alam"   

3)
"Kuna nuru kubwa katika Swalah ambayo inaangaza ndani ya nyoyo za wale wanaoimarisha swala na wale wanaomakinika na kunyenyekea kwenye Swalah zao. Kwa hivyo, ukija kuswali, komboa moyo wako kutokana na dunia na vilivyomo ndani yake; jihusishe na kumakinika na hudhurio la Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)   Ambaye Swalah hiyo ni kwa ajili Yake.  Lazima ujue kwamba msingi wa Swalah ni unyenyekevu na kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  kwa kusimama, kurukuu, na kusujudu mbele Yake, na Kumtukuza kwa takbir, tasbih, na dhikri.
Kwa hivyo tunza Swalah yako kwa sababu ni ibada kubwa kabisa miongoni mwa ibada. Usimuache shetani acheze na moyo wako na kukupurukusha katika Swalah ili usipate utamu wa nuru ya Swalah. Na muombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwani Yeye ndiye Mbora wa Wasaidizi".

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atujaaliye tuwe miongoni mwa waja wake ambao wanathamini ile zawadi Aliyotupa ndani ya Swalah. Tunamuomba Atuongezee unyenyekevu na utulivu ndani ya Swalah ili tuwe ni wenye kufaidika nayo. Tunaumuomba Allaah Atulete pamoja ndani yake (Swalah) na atuzidishie idadi ya safu na atupe nguvu ndani yake (Swalah) ili tutoke ndani yake ilihali tumenufaika. Aamiyn.

بسم الله الرحمن الرحيم
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
 أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ فَاسِقُونَ 
Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa dhikri[1] ya Allaah na (kwa) yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawarefukia muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki (Al-Hadiyd: 16)
Ramadhaan inakaribia si chini ya miezi miwili! Umefika wakati kwa wale waliozama katika shirki, pombe, (kila aina ya) madhambi na bid’ah, kujirekebisha na kujitakasa kwa Tawhiyd, utiifu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) na kufuata Sunnah ya Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa hiyo:
  • Tujirekebishe kuanzia sasa ili itakapoingia Ramadhaan, nyoyo na viungo vyetu viwe vinamwabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Pekee bila ya kumshirikisha.

  • Tujirekebishe sasa ili itakapoingia Ramadhaan, viungo vyetu vitende amali zenye kumridhisha Allaah!

  • Tujirekebishe sasa ili inapoingia Ramadhaan, vitendo vyetu viendane sawa na Sunnah ya mpenzi wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ili tuwe ni wenye kuwafuata Maswahaba (Radhiya Allaahu 'anhum) ambao ni viumbe bora kabisa baada ya Mitume.

Kujirekebisha na kujitakasa kunahitaji muda, na hakuna muda mzuri kama huu unaokaribia mwezi wa Ramadhaan!
Salafus-Swaalih walikuwa wakiitarajia Ramadhaan na wakijitayarisha mapema mno. Walikuwa wakiiomba du’aa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Awawezeshe kuifikia Ramadhaan.
Vipi basi wewe? Umefikia wapi katika kutarajia, kujitayarisha na kuomba du’aa?
Au utakuwa miongoni mwa wale wajinga wanaosubiri siku ya kwanza ya Ramadhaan ndio uanze kupapatika kurekebisha nafsi yako hali ya kuwa bado umezamia katika shirki, madhambi na bid’ah? Matokeo yake basi ni kwamba mwezi utakapomalizika utakuwa bado una athari za maovu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّهِ ثُمَّ تُوَفَّى كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Na iogopeni Siku mtayorejeshwa humo kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa. (Al-Baqarah: 281)
Na Anasema pia:   
وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَى فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَى 
Ama yule aliyekhofu kisimamo cha Mola wake, na akaikataza nafsi yake na matamanio. Basi hakika Jannah (itakuwa) ndio mahali pake pa kukimbilia. (An-Naziaat: 41)
Na Anasema pia:
أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ فَاسِقُونَ 
Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa dhikri[2] ya Allaah na (kwa) yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawarefukia muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki (Al-Hadiyd: 16)

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuongoze sote na ndimi zetu zinazosema: “Tunaitaka Ramadhaan na tunaipenda” huku (niyyah zetu na) vitendo vyetu ni kinyume chake. Na uhakika wenyewe ni kwamba wako wanaosema: “Hatupendi Ramadhaan! Isitufikie! Hatutaki kuzindukana madhambi yetu na maasi! Hatutaki kuathirika tukatoka kwenye shirki, bid’ah na dhambi na hali tumeshaizoea! Tafadhali msitukere!
 Ndugu yetu Muislamu! Anza haraka kujitakasa ili Ramadhaan itakapoingia, moyo wako na viungo vyako viweze kukubali kwa sahali kutekeleza kheri nyingi. Hivi ndivyo mtu anavyojitayarisha kikweli na ndipo atakapofaidika na mwezi mtukufu wa Ramadhaan.
ZANZIBAR.

KAMPUNI `YA KIJANI YA AGRO LIMITED YENYE MAKAO MAKUU YAKE NCHINI ISRAEL IMEKUSUDIA KUANZISHA KILIMO CHA MAZAO YA MBATATA NA VANILLA KWA KUTUMIA MFUMO WA TEKNOLOJIA YA KISASA UTAKAOSHIRIKISHA VIJANA WAZALENDO HAPA NCHINI.


UONGOZI WA KAMPUNI HIYO PIA UMEJIPANGA KUTOA MAFUNZO MAALUM KWA VIJANA KATIKA SEKTA YA KILIMO KWA KUWAJENGEA UWEZO WA UZALISHAJI WA MAZAO TOFAUTI YATAKAYOWAPA FURSA YA AJIRA BADALA YA KUSUBIRI AJIRA YA SERIKALI.


MWAKILISHI WA KAMPUNI HIYO YA KIJANI AGRO LIMITED YENYE TAWI LAKE MJINI DAR ES SALAA NA MKOANI IRINGA BWANA RONEN ALMOG AMEELEZA HAYO WAKATI WA MAZUNGUMZO YAKE NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI OFISINI KWAKE VUGA MJINI ZANZIBAR.


AMESEMA KUWA UONGOZI WAKE UTAJITAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUPITIA WIZARA YA KILIMO HUSUSAN KATIKA KUWAPATIA WAKULIMA TAALUMA YA KILIMO.


AMEELEZA KUWA KITUO MAALUM CHA MAFUNZO YA KILIMO KITAANZISHWA ILI KUWAPA FURSA KUBWA WAKULIMA NA KUJIFUNZA MBINU ZA KISASA ZA KILIMO KWA LENGO LA KUENDELEZA SEKTA HIYO KATIKA MFUMO WA KITEKNOLOJIA.
AKITOA SHUKRANI ZAKE MAKAMO WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AMESEMA KUWA KILIMO BADO KITAENDELEA KUWA SEKTA MAMA KWA UCHUMI WA ZANZIBAR AMBAPO KIMEKUWA KIKITOA AJIRA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 70%.


BALOZI SEIF AMESEMA KUWA MBATATA NA VANILA NI MAZAO YANAYOHITAJIKA ZAIDI HAPA ZANZIBAR KUTOKANA NA ONGEZEKO KUBWA LA HOTELI ZA KITALII ZILIZOPO SEHEMU MBALI MBALI MIJINI NA VIJIJINI.


MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ALIUPONGEZA UONGOZI WA KAMPUNI HIYO KWA UAMUZI WAKE ILIYOCHUKUWA WA KUTAKA KUSAIDIA MIRADI MBALI MBALI YA KILIMO HAPA ZANZIBAR.
PEMBA.

MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA DADI FAKI DADI AMESEMA KUWA TATIZO LA UPUNGUFU WA WALIMU NA MADAKTARI LITAENDELEA KUZIKABILI NCHI ZINAZOENDELEA KUTOKANA NA ONGEZEKO LA WATU KATIKA NCHI HIZO LINALOSABABISHWA NA KUTOZINGATIWA SUALA LA UZAZI WA MPANGO .

DADI AMETOA KAULI HIYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZAZI , WANAFUNZI NA WALIMU WA SKULI ZA SEKONDARI ZA CHWAKA TUMBE , KINOWE NA TUMBE WAKATI WA ZIARA YAKE YA KUHAMASISHA MAENDELEO YA ELIMU KATIKA MKOA HUO .

AMESEMA KUWA IWAPO JAMII HAITAZINGATIA NA KUTOA KIPAOMBELE SUALA LA UZAZI WA MPANGO TATIZO HILO LA UPUNGUFU WA WALIMU NA MADAKTARI LITAENDELEA KUZIKABILI SEKTA YA ELIMU NA AFYA KATIKA NCHI HIZO IKIWEMO ZANZIBAR.

AMEWATAKA WAZAZI KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUKABILIANA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA WALIMU KATIKA SKULI ZAO PAMOJA NA KUWATUMIA VIJANA WALIOMALIZA VYUO VIKUU WALIOMO KATIKA MAENEO YAO .

AWALI MKUU HUYO WA MKOA ALIITAKA WIZARA YA ELIMU MKOA HUMO KUANDAA MIPANGO MADHUBUTI ITALAYO FANIKISHA KUPATIKANA KWA WALIMU WA MASOMO YA BIOLOGY NA PHYSICS KATIKA SKULI YA TUMBE NA CHWAKA .

KWA UPANDE WAKE AFISA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI MKOA WA KASKAZINI PEMBA NDUGU HASSAN SHEHA AMEWATAKA WAZAZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU KATIKA KUTAFUTA NJIA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO .
WILAYA YA MJINI.

WAISLAMU WA ZANZIBAR WAMETAKIWA KUCHAGUWA WACHUMBA WENYE KUFUATA VIGENZO ALIVYOVIWEKA BWANA MTUME MUHAMMAD (SAW) ILI KUWEPUKANA NA TALAKA ZISIZOKUWA ZA LAZIMA.

KAULI HIYO IMETOLEWA NA USTADH SUBUKI PANDE SUBUKI WA BUBUBU ZANZIBAR WAKATI ALIPOKUWA AKIZAUNGUMZA NA RADIO ADHANA FM KATIKA KIPINDI CHA WAJIBU WANGU KUSEMA KINACHOENDESHWA NA RADIO ADHANA FM.

AMESEMA KUWA SABABU ZINAZOPELEKEA KUVUNJIKA KWA NDOA NI WAZAZI KUWAOZESHA WATOTO WAO BILA KUZ`INGATIA VIGENZO ALIVYOVITOA BWANA MTUME MUHAMMAD (SAW).

AKIELEZEA KWA UPANDE WA VIJANA AMESEMA KUMEKUWA NA BAADHI YA VIJANA WAMEKUWA WAKIOA KWA KUANGALIA UZURI WA SURA,KITU AMBACHO NI KINYUME NA VIGENZO ALIVYOVITOA MTUME (SAW) VYA KUTAFUTA MCHUMBA NA KUPELEKEA KUONGEZEKA KWA TALAKA ZA KIHOLELA.

KUTOKANA NA HALI HIYO AMEWATAKA WAZAZI NA VIJANA KUFUATA MISINGI ANAYOIRIDHIA MWENYEZI MUNGU KATIKA KUTAFUTA MCHUMBA.
Next PostNewer Posts Previous PostOlder Posts Home