zanzibar.

makamo wa kwanza wa rais wa zanzibar maalim seif sharif hamad, ameelezea kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi mitatu inayoendelea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa abeid amani karume.

miradi hiyo inahusisha ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege, ujenzi wa uzio wa eneo la uwanja wa ndege, pamoja na ujenzi wa jengo jipya la abiria (terminal 2).

akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi hiyo huko uwanja wa ndege wa zanzibar, maalim seif amesema kuwa hatua iliyofikiwa inatia moyo, na kuwataka wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo  kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati.

amesema kuwa serikali kwa upande wake itaweka mkakati wa makusudi ili iweze kumaliza kuwalipa fidia wananchi ambao bado hawajalipwa, na kuruhusu ujenzi wa uzio uweze kukamilika kwa wakati.

mapema meneja wa mradi wa ujenzi wa uzio huo bw. frederick nkya, alimueleza makamo wa kwanza wa rais wa zanzibar kwamba hadi sasa tayari asilimia 73 ya ujenzi huo imeshakamilika.

hata hivyo amesema changamoto kubwa inayowakabili ni eneo la mita elfu tatu na mia moja ambapo sehemu kubwa ya eneo hilo bado wananchi hawajalipwa fidia.

amefahamisha kuwa hadi sasa eneo la mita elfu mbili na mia saba ndilo ambalo halijafanyiwa tathmini kuweza kuwalipa wananchi walioko katika maeneo ya mradi huo.



miradi ya ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka (taxiway) pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege (apron) katika uwanja huo inafadhiliwa na benki ya dunia pamoja na serikali ya mapinduzi ya zanzibar, ambapo mradi wa ujenzi wa uzio wenye urefu wa mita 11,690  katika uwanja huo, unatekelezwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar pekee, ambapo zaidi ya shilingi bilioni sita zitatumika hadi kukamilika kwa mradi huo.

akizungumzia mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria meneja wa mradi huo ndugu ibrahim zhang amesema kuwa ,kazi hiyo sasa inaendelea vizuri.


mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria awali ulitiwa saini mwezi wa septemba 2009 kati ya wizara ya miundo mbinu na mawasiliano na kampuni ya ujenzi ya beijing construction engineering group ya china, lakini baadae serikali iligundua kuwa ukubwa wa jengo uliopendekezwa mwanzo haukidhi haja.

hata hivyo kufuatia kasoro hiyo serikali ilikubaliana na mkandarasi kuongezwa ukubwa wa jengo kutoka mita 15,600 hadi mita 17,800 kwa ongezeko la fedha dola za kimarekani milioni 11 nukta 8, na kufanya gharama za mradi huo kufikia dola la kimarekani milioni 82 nukta 2.


Na Miza Othman-Maelezo Zanzibar           27/ 3 /2014 
                               
Wizara  ya Kilimo na Uvuvi Zanzibar Imeishukuru Serikali ya Japan kwa kuamuwa  kuwajengea Soko la kisasa  kwa lengo la kuimarisha na kuleta maendeleo  hapa Zanzibar

Mkataba huo umetiwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya KilImo na Uvuvi Dr. Kassim Gharib pamoja na Meneja  wa Fisheries Engineers Company Of Japan, Tadashi Ogawa huko  Afisini kwake Maruhubi Mjini Zanzibar ikiwa ni njia moja ya kuleta ushirikiano.

Amesema  huu ni wakati muwafaka kwa kujitokeza  Meneja  huyo kutokana na kutokuwepo kwa soko la uhakika  ambalo litakaloweza kuhifadhi samaki wengi wanaovuliwa hapa Zanzibar.

Aidha Dr. Kassim amesema  hii ni njia ya  kuiimarisha Serikali na kuwaletea  maendeleo Wavuvi katika ufanyaji wakazi  zao hasa kwa kipindi kigumu walichonacho.

Hata hivyo amesema kuwa faraja hiyo haitowanufaisha  wavuvi tu  bali na Wananchi  kwa ujumla hasa wakati wanapohitaji  kitoweo cha haraka katika Mji wao wa Zanzibar.



Vilevile amesema  hadi hivi sasa bado hajapatikana Mkandarasi  atakaeweza kusimamia soko hilo lakini  endapo ikiwa tayari  itatangazwa tenda na kuweza kupatikana kwa haraka.

Amewashauri wananchi wanaolitumia soko hilo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na  kwa lengo la kuwaletea faraja soko hilo.

Dr. Kassim Gharib amesema  katika ujenzi wa Soko hilo litagharimu Sh. Bilion 14 hadi  kumaliza kwake. 
                                         
           IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR





na harith subeit

zanzibar.

kesi inayowakabili viongozi wa jumuiya na taasisi zakiislam zanzibar imeakhirishwa hadi julai 3 mwaka huu ambapo imewekewa pingamizi na mkurugenzi wa mashtaka kuhusu dhamana iliyotolewa kwa washtakiwa hao.

mapema muendesha mashitaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka dpp raya mselem aliwasilisha pingamizi ya kupinga uamuzi wa mahkama kuu kusikiliza ombi la dhamana ya watuhumiwa hao.

licha ya mahakama kuu kutoa dhamana kwa watuhumiwa bado upande wa mashtaka unapinga suala hilo na umeamua kukata rufaa ili washtakiwa warejeshwe tena rumande baada yakukaa ndani mwaka mmoja na miezi minne.

hata hivyo wakili wa upande wa utetezi abdalla juma ameiomba mahkama hiyo kuakhirisha shauri hilo hadi mahakama ya rufaa itakapokaa na kusikiliza rufaa hiyo.

hata hivyo jaji isack sepetu hakupingana na hoja hiyo.

watuhumiwa waliofika mahakamani leo ni pamoja na amiri mkuu wa jumuiya ya maimamu zanzibar samahatu sheikh farid hadi ahmed,amiri mkuu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar fadhilatu sheikh mselem bin aly, naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar zanzibar al-ustadh azan khalid hamdan.

wengine ni katibu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar al-ustadh abdalla saidi, maustadh mussa juma mussa, suleiman juma sleiman, khamis ali sleiman, hassan bakari sleiman, gharibu ahmada juma, na majaliwa fikirini majaliwa.

mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu mali, uchochezi,ushawishi , kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa
kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne al-ustadh azan khalid ambae anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo vinaweza v kusababisha uvunjifu wa amani.

vitendo hivyo vinadaiwa kufanyika kati ya oktoba 17,18 na 19 mwaka ,2012 katika maeneo tofauti katika manispaa yaa mji wa zanziba ambapo washitakiwa hao wote wamekana makosa yote hayo.

viongozi hao walipewa dhamana na mahakama kuu ya zanzibar tarehe 27 mwezi wa pili mwaka huu baada yakutekeleza masharti yaliyowekwa.


ZANZIBAR.

VIJANA NCHINI WAMESHAURIWA KUTUMIA FURSA ZA KUJIPATIA TAALUMA KATIKA NYANJA MBALI MBALI KUTOKA KATIKA VYUO NA TAASISI ZA ELIMU HAPA NCHINI ILI VIWAJENGEE UWEZO WA KUJITEGEMEA WENYEWE KIMAISHA.

 

USHAURI HUO UMETOLEWA  NA  WALIMU WA VYUO NA TAASISI MBALI MBALI HAPA ZANZIBAR KATIKA KONGAMANO LA VIJANA WENYE TATIZO LA AJIRA NCHINI HUKO KATIKA UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZAMANI, KIKWAJUNI MJINI HAPA WAKATI WAKIWASILISHA MAELEZO KUHUSIANA NA KUJIUNGA, TAALUMA WANAZOZITOA, MAHITAJI YA SOKO YA FANI HUSIKA NDANI NA NJE YA NCHI, ADA INAYOHITAJIKA  ILI KUWAJENGEA UWELEWA NA KUCHUKUA HATUA ZA MAAMUZI SAHIHI YA KUJIKWAMUA KIMAISHA.

 

WALIMU HAO KUTOKA  TAASISI YA SAYANSI NA TECHNOLOGIA KARUME, CHUO CHA SAYANSI YA AFYA MBWENI,KITUO CHA UFUNDI MKOKOTONI, CHUO CHA MAENDELEO YA UTALI ZANZIBAR,KUMBU KUMBU YA MWALIMU NYERERE, UONGOZI WA FEDHA CHWAKA,ZANZIBAR SCHOOL OF HEALTH (SHAA) MOMBASA PAMOJA NA TAASISI YA BUISSNESS & TECHNOLOGY MWANAKWEREKWE WAMESEMA KUWA NI LAZIMA VIJANA KULIWEKA SUALA LA ELIMU MBELE ILI WAPATE TAALUMA HUSIKA KWA MAENDELEO YAO NA TAIFA KWA JUMLA.

 

VIONGOZI HAO WAMEWAOMBA VIJANA KUJIUNGA NA VYUO NA TAASISI HIZO KWA GHARAMA NAFUU ILI KUJINUFAISHA HIVI SASA NA HAPO BAADAE.

 

NAO VIJANA HAO KUTOKA SEHEMU MBALI MBALI NCHINI WAMEISHUKURU JUMUIYA YA MAENDELEO  YA VIJANA WA MIKUNGUNI (MYDO) KWA KURATIBU KUWEPO KWA KONGAMANO HILO AMBALO LIMEWAPA FURSA NZURI  YA KUPATA UWELEWA NA KWAMBA SUALA LA ELIMU KWA AJIRA WATALIFANYIA KAZI IPASAVYO KUILINGANA NA HALI ZAO ZA KIFEDHA.
Next PostNewer Posts Home